Latest Updates

Justin Bieber atoa msaada katika ajali ya gari iliyowahusisha watoto wa Mayweather


Justin Bieber aambaye amewahi kuingia katika matukio ya ajali ya gari mara kadhaa, Jumapili iliyopita aligueka kuwa msamalia mwema na kutoa msaada wa haraka kwa watoto wa bondia Floyd Mayweather waliopata ajali ya gari.
Kwa mujibu wa TMZ, muda ambao watoto hao wanapata ajali ya gari huko Los Angeles, Floyd alikuwa kwenye tukio la red Carpet ya tuzo za BET na alipewa taarifa kwa njia ya simu na Justin Bieber.
Inaelezwa kuwa magari mengi yaligongana katika eneo hilo na kuhusisha gari walilokuwemo watoto wa Mayweather.
Justin alikuwa katika eneo hilo na alikimbia kwenye tukio hilo na kuwachukua watoto hao haraka na aliwaeleza polisi kuwa ni watoto wa rafiki yake.
Watoto hao hawakupata majeraha makubwa, mtoto mmoja alichanika kidogo kwenye mdomo wa chini na Justin aliamua kuwafariji kwa kuwaimbia wimbo wake mpya kabla hajawapeleka kwa baba yao.
Inaelezwa kuwa baada ya kuwafikisha watoto hao kwa Floyd. Justin alirudi katika eneo hilo na kuwaarifu polisi kuwa watoto hao wameshafika kwa baba yao.

0 Response to "Justin Bieber atoa msaada katika ajali ya gari iliyowahusisha watoto wa Mayweather"

Post a Comment