Latest Updates

DR.DRE AINGIA MKATABA WA APPLE


HATIMAYE yale mazungumzo yaliyokuwa yanasubiliwa muda mrefu kuhusiana na dili iliyokuwa inasubiliwa kwa hamu, kutoka kwenye  kampuni ya kielektroniki ya Apple imethibitisha kuwa itanunua kampuni ya Beats Electronics watengenezaji wa headphones za Beats by Dre na bidhaa nyingine za muziki inayomilikiwa na mwanamuziki Dr. Dre.

Dili hiyo ambayo ina thamani ya jumla ya dola bilioni 3 inadaiwa kuwa ndio dili kubwa zaidi kubwa ya manunuzi kuwahi kufanywa na kampuni ya Apple. 

Ikiwa ni sehemu ya manunuzi, wagunduzi wa kampuni hiyo Jimmy Iovine na Dr Dre wataungana na kampuni ya Teknolojia duniani Apple. 

Bosi wa kampuni ya Apple Tim Cook amesema dili hiyo itaruhusu kampuni ya Apple kutengeneza bidhaa nzuri zaidi za muziki kupitia ugunduzi uliofanywa, teknolojia inayokuwa kwa kasi duniani.

0 Response to "DR.DRE AINGIA MKATABA WA APPLE "

Post a Comment