Latest Updates

Mjadala: Skywalker, Jabir Saleh na Raheem Da Prince wanavyoichukulia diss ya Jay Z kwa Drake 'Miss Dreezy' (Audio)


March 23 ilikuwa ni siku ya mshituko kidogo na minong’ono kwa watu wengi wanaofuatilia hip hop duniani baada ya kuachiwa wimbo wa Jay Electronica ‘We Made It’ aliomshirikisha Jay Z ambapo Jay Z alisikika akimchana Drake kwa kumtaja jina na kumfananisha na mwanamke ‘Mrs Dreezy’.
“Sorry Mrs. Drizzy for so much art talk” msitari ambao ulizua mengi.
 “Silly me, rapping ‘bout sh*t tha I really bought/ While these rappers rap about guns that they ain’t shot/ And bunch of other silly sh*t that they ain’t got.” Alirap Jay Z.
Mistari hiyo ni matokeo ya kile kilichoandikwa na Rolling Stone na kumnukuu Drake akieleza kuwa Jay Z hawezi kwenda mistari kadhaa bila kuongelea sanaa za uchoraji.
“It’s like Hov can’t drop bars these days without at least four art references, I would love to collect (art) at some point, but I think the whole Rap/ art world thing is getting corny.” Alikaririwa Drake ambaye hata hivyo baadae alikanusha kusema hivyo.
Tumejaribu kupata maoni ya watu ambao ni miongoni mwa wafuatiliaji wa hip hop na mikasa yake duniani ili kujadili kile ambacho kilikuwa mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii hasa kwa kuzingatia ukubwa wa Jay Z, ukaribu aliokuwa nao kwa Drake na jinsi react na kumchana kwa kumtaja jina.
Fredrick Bundala aka Skywalker, mhariri mkuu wa mtandao wa Bongo 5, Jabir Saleh au Kuvichaka ambaye ni mtangazaji wa The Jump Off na Bongo Dot Home wa 100.5 Times F na Raheem Da Prince ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha The Switch cha Times Fm wametoa mitazamo yao kuhusu hilo kwenye mjadala huu au discussion kwa lugha ya kigeni.
Jabir Saleh yeye ameeleza kuwa hakutegemea kabisa kuwa Jay Z kwa jinsi alivyo mkubwa kimuziki angeweza kumchana Drake kwa kumtaja jina, lakini pia ametoa mapendekezo yake kuwa huenda Jay Z angetumia njia tofauti kufikisha ujumbe wake.
“Sikuwa nategemea labda Jay Z angeweza kumjibu Drake kwa mtindo ule, nilifikiri kwamba labda Jay Z angetumia Sanaa zaidi. Kwa jinsi alivyofanya ni kama kutukana, kumfananisha mwanamme na mwanamke ni kumkashifu, kwa hiyo amemkashifu.” Ameeleza Jabir Saleh.
“Ukiangalia lugha aliyotumia Drake ilikuwa sio lugha ya matusi, alisema kwamba jamaa hawezi kwenda bars zaidi ya nne asizungumzie sanaa za uchoraji, kuwataja wachoraji.” Ameongeza.
Jabir ameeleza kuwa alishaongea na watu kadhaa ambao ni wafuatiliaji wa wa masuala ya hip hop na wakasema Drake alisema ukweli kwa kuwa nyimbo nyingi za Jay Z anazungumzia sanaa ya uchoraji na mfano mkubwa ni wimbo wa Picasso.
Jabir anaamini kuwa Drake aligusa kidonda cha Jay Z katika hilo kwa kuwa alisema ukweli, alisema mapungufu ya Jay Z na ndio sababu ikamuuma na kuamua kujibu, “to me Drake is a winner halafu Jay Z amepanic, yaani hakustahili labda kuzungumzia hivyo.” Huo ni mtazamo wa Kuvichaka.
Kwa upande wa Fredrick Bundala aka Skywalker, yeye ameelezea kuhusu ukaribu wa Drake na Jay Z na mategemeo ya wengi kuwa kuna kitu kizuri kinakuja kati yao lakini mwisho wa siku ikawa surprise ya mtafaruku usiotegemewa.
“Kwa sababu tunajua ukaribu uliopo kati ya Drake na pamoja na Jay Z. unajua kuna wakati mpaka walikuwa wanahisi kwamba Jay Z anaweza kumsaini Drake kwenye Roc Nation. Hivi karibuni pia hizo rumors zilikuwa zimerejea, niliona juzi Allhiphop.com waliandika kwamba kuna kitu ambacho kinaendelea kati ya Jay Z na Drake kumuweka Roc Nation.
“Kwa hiyo Ilikuwa kama surprise unajua baada ya kuona kwamba Jay Z amemgeukia tena Drake kwa kile ambacho alikisema.” Ameeleza Skywalker.
Skywalker hakuwa mbali na Jabir Saleh kuhusu Jay Z kumuita Drake ‘Mrs Dreezy’, na kwamba anaamini hicho kitamkera Drake.
“Ile verse ambayo imemtaja pia Drake kwenye hii remix ya ‘We Made It’ unajua haijamtarget Drake tu. Sawa kwenye ule msitari…kwanza kibaya zaidi amemuita Drake Mrs., pengine hiyo Drake itamkera kidogo kwanza kwa nini amuite Drake Mrs Dreezy. Hata kwenye discussion nyingi nimeona hiyo kitu imeleta shida kidogo, watu wameiona sana hiyo.” Sky ameeleza.
Ameongeza kuwa hata kwenye rapgenius ambao huwa wanatafsiri maana ya mashairi ya nyimbo nyingi wao wameeleza maana ya mistari ambayo ameitaja Jay Z mbali na hiyo ‘Mrs’, mistari anayoeleza kuwa yeye ni tofauti na rappers wengi ambao warap kuhusu bunduki ambazo hawajazitumia kushut lakini yeye anazungumzia vitu ambavyo anavyo.
“Kwenye rap genius ambao waga wana-translate lyrics maana yake kuna watu wamediscuss, maana yake anachosema ni kwamba unajua rappers wengi sasa hivi ana single moja anaanza kuimba kuhusu  I’m living in the cribs yaani nyumba nzuri nzuri, I get cars I get money lakini kumbe wanazungumzia fantasy tu, yaani ndoto tu ambazo hawajasifikia bado. Lakini Jay Z yeye anavyoviimba ni vitu ambavyo anavyo.
“Tunafahamu kwamba Jay Z katika list ya Forbes ya wasanii watano wenye pesa yeye yumo nyuma ya Diddy. Yaani ni verse ambayo ameitumia kuwakumbusha vijana kwamba guys mimi ni Jay Z, I’m Hov. Yaani ukilinganisha na mafanikio niliyokuwa nayo hapa nyie bado mno.” Amefafanua Skywalker.
Hata hivyo, Sky anaamini hiyo pia kwa Drake ni sehemu ya ‘kick’ na kwamba anatarajia kitu kizuri kinakuja kati ya Drake na Jay Z hivi karibuni licha ya kuwepo hizo tofauti.
“Mimi nahisi kuna kitu kitakuja, na nina feelings kwamba kuna kitu ambacho jamaa wanakitengeneza pia. Sitaki kuamini kama ni ule ugomvi au beef tunazosikia kati ya Rick Ross na akina 50…kwa sababu naamini Jay Z alisikia Drake akisema ‘guys sikusema hayo maneno’. Naamini alisikia, sasa kama alisikia kwa nini Jay Z bado achukulie maneno ya Drake ambayo alisema hakuyasema kama serious kiivo!? Nahisi Jay Z aliisema ile ki-metaphor tu, yaani ile kuchangamshana. Ni kama alivyofanya Kendrick Lamar kwenye Control. Sio kwamba aliowataja mule anawachukia wala nini. Ni katika kuchangamsha tu.” Ameeleza.
Amesisitiza kuwa yeye anaiona positive zaidi ya vile wengi walivyoichukulia negatively.
The King Of Entertainment shows kama anavyojiita, Raheem Da Prince ambaye pia ni C.E.O wa Swahili Nation, yeye anamuunga mkono Drake kwa kile kilichosemekana alikisema kuhusu Jay Z kwa kuwa ni sehemu ya utamaduni wa hip hop kusema ukweli. Lakini pia anaamini Jay Z hajakosea, so ni kama win-win situation.
Raheem anaungana na Jabir Saleh kiasi fulani kuwa kilichosemwa ni ukweli.
 “Ningependa tu kuwatoa wasiwasi mashabiki wa hip hop duniani wa Drake pamoja na Jay Z. Tukumbuke kwamba hip hop ni utamaduni, maana yake unaongea ukweli haijalishi huyu ni mshikaji wangu haijalishi huyu ni aduni yangu.” Anaongea Raheem
“Na Drake alichokifanya ni kuongea mawazo yake anahisi nini Jay Z anakifanya, ni comments tu amezitoa. Hip hop sio kusema kwamba Jay Z is the greatest rapper of all the time wakati unajua kabisa kuna kitu fulani anakosea au kuna kitu fulani anaenda sio. Na Jay Z alichokifanya sio kibaya. Amejibu comment ya Drake kwenye ngoma, ina maanisha kuwa yeye ni msanii wa hip hop na anafahamu nguzo za hip hop zinataka nini.”
Hata hivyo, Raheem anatofautiana na wengi kimtazamo kimtazamo kuhusu neno ‘Mrs Dreezy’ na anaamini Hov hakulitaja hilo neno kwenye wimbo ule ule ambao wengi tumeusikiliza.
“Actually hakusema Miss Dreezy wala Mrs. Dreezy, wala haikuwa ni insult wala tusi. Alisema Mr. Dreezy kwa hiyo hakukosea. Unaweza kulinganisha na ile kesi ya 50 Cent, Diddy, Rick Ross na Steve Stoute. 50 Cent alitoa mawazo yake kwa mfano juu ya comments za Steve Stoute na pia walishakutana kabisa kwenye NBA game wakaongea. 50 akamwambia Steve unahitaji kuni-   apologize kwa sababu umefanya hiki na kile. Hip hop inatakiwa iwe hivyo kwamba una kitu moyoni kiseme. Uwasilishaji wake ndio unaweza kuleta beef ama usilete beef. Lakini Jay Z hakutukana na wala Drake hakutukana.”
Raheem ameungana na mawazo ya Skywalker kuwa kuna kitu kinakuja kati ya Jay Z na Drake, na ameenda mbali na kusema kuwa tegemea wimbo wa pamoja kati yao.
“Tarajia kupata ngoma mpya ya Drake na Jay Z! Ukasema nilikuwa nao studio Roc Nation, no. mimi naongelea kwa mtazamo, naongelea kwa jinsi game inavyokwenda. Hawa jamaa ni watu wawili ambao wanajielewa sana. Mimi sisemi ni shabiki mkubwa wa Jay Z ama Drake, lakini kwa jinsi hawa jamaa ngoma zao na mawazo yao kwenye interviews na historia zao hawa wawili hawa ni watu ambao wanajielewa sana. So, don’t expect any beef it’s all about peace and love na mawazo chanya.”
Huu ndio mtazamo wa Jabir Saleh, Skywalker na Raheem Da Prince. Huenda kweli kuna kitu kinakuja kati ya wawili hawa…nobody knows.
Unaweza kutoa mtazamo wako pia.
Wasikilize hapa:http://www.hulkshare.com/tpd6asc9y60w

0 Response to " Mjadala: Skywalker, Jabir Saleh na Raheem Da Prince wanavyoichukulia diss ya Jay Z kwa Drake 'Miss Dreezy' (Audio) "

Post a Comment