Latest Updates

TAZAMAPICHA NYUMBA IKITEKETEA KWA MOTO MWANZA CHANZO JIKO LA GESI


Mwananchi juu ya paa la nyumba ya mtu mmoja maarufu kwa jina la Mama Mayunga, akijaribu kurusha vifuko vya mchanga katika moja ya majengo ya nyumba iliyozuka moto Jana majira ya saa 5 asubuhi mtaa wa Majengo jirani na Masangwa Guest House wilayani Misungwi mkoani Mwanza. 
Moto huo unaotajwa chanzo chake kusababishwa na jiko la gesi ulilipuka na kuiteketeza kabisa nyumba hiyo ikiwa na furniture zake.
Huku baadhi yao wakiwa wamejitosa kufanya uokoji wa mali, wananchi wengine kama kawaida yao walikimbilia  eneo la ajali kushuhudia moto huo uliokuwa ukivuma kuashiria hatari na eneo hilo si salama. 
Moto ukipamba moto na kutokea kwenye madirisha ukivuma. 
Ingawa jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kuwasihi wananchi kusogea mbali toka eneo la moto kwani chanzo chake ni moto wa gesi katu watu hao hawakutii amri  hiyo zaidi ya kuusogelea zaidi.
Hali ndiyo ilivyokuwa huku wananchi hao wa wilaya ya Misungwi wakisubiri huduma ya zimamoto toka magari ya Halmashauri ya jiji la Mwanza, umbali wa dakika 45.
Hali tete.
Saa moja baadaye gari la zimamoto lilifika eneo la ajali ya moto lakini hata hivyo liliambulia kuzima magofu huku milango, madirisha na mali zilizokuwa kwenye nyumba hiyo zikiteketea kabisa. (picha na Wiliam Bundala wa kanda ya Ziwa)

0 Response to "TAZAMAPICHA NYUMBA IKITEKETEA KWA MOTO MWANZA CHANZO JIKO LA GESI "

Post a Comment