Latest Updates

"Ni kweli nipo na Diamond, napenda wanaume weusi" - Wema Sepetu


Mwanadada Wema Sepetu ambaye pia aliwahi kuwa Miss Tanzania 2006 ambaye kwa sasa anaendesha kampuni yake binafsi iitwayo Endless Fame inayojishughulisha zaidi na utengenezaji wa Filamu mbalimbali.

Kupitia kipindi cha Leo tena February 28 Wema Sepetu amekubali kutaja sifa za mwanaume anayempenda kuwa na mvuto kwake,swali lililoulizwa na Watangazaji wa kipindi hicho ni kuhusu mwanaume wa sifa gani anayedhani anaweza kuolewa nae ambapo Wema alijibu “Kuolewa sio shida je huyo mwanaume nampenda,maana naweza kuja kuchumbiwa lakini nisimpende”

“Mimi nampenda Mwanaume mweusi,wanaume weupe sio kwamba sijawahi kuwa nao lakini nakuwa sina mzuka nao”.

Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Diamond amekiri kwa kusema’Kweli niko na Nasib - Diamond na nadhani muda huu kutakua na utulivu ndani yake,ule utoto tuliokua tunafanya nadhani ulikua utoto na imekua Power Couple toka mwaka 2010 kwa hiyo tuna ni miaka 4 sasa,kwa sasa tumeamua kuwa serious’.
Habari kwa Hisani ya Millard Ayo
Wema Sepetu pia kaandamana na Ant Ezekiel kwenye interview ya kipindi hicho kinachorushwa na Clouds Fm.

0 Response to ""Ni kweli nipo na Diamond, napenda wanaume weusi" - Wema Sepetu"

Post a Comment