Latest Updates

Miley Cyrus awatemea maji mashabiki kwenye tamasha lake


Miley Cyrus, ambaye kila anapopanda jukwaani hufanya vituko vya aina yake ambavyo huzua hisia tofauti, Alhamisi wiki hii akiwa kwenye tamasha la ziara yake ya Bangerz, aliwatemea maji mashabiki wake wa Tampa, Florida.
Mwimbaji huyo alikuwa anazunguka jukwaani akiwa ameshikilia chupa ya plastic yenye maji huku akizungumza na mashabiki hao waliolipa kiasi kikubwa cha pesa na bila ya wao kutarajia aliwatemea maji baada ya kupiga ‘pafu’ ili kutunza maji mengi iwezekanavyo kwenye mashavu yake.
Hata hivyo, mashabiki walionekana kukichukulia poa kitendo hicho na kuendelea kumpigia shangwe za kutosha wakati akitema maji hayo mara kadhaa kuelekea kwao.

0 Response to " Miley Cyrus awatemea maji mashabiki kwenye tamasha lake"

Post a Comment