Latest Updates

DJ K-FLIP MWENYE SHAHADA YA FEDHA NA UCHUMI ALIYEBOBEA KATIKA MASWALA YA MUZIKI


Miaka ya nyuma baadhi ya watu walikuwa wanaamini kuwa Yule anayepiga muziki au kwa jina linalofaamika sana ‘DJ ‘ katika ukumbi za starehe usiku maalufu kama ‘Disko’ ni muhuni na hana elimu ya kutosha

DJ K-Flip ni mmoja wa kundi la Madj wa Pro -24 ambaye yeye anaonyesha utofauti wa dhana hiyo waliyonayo baadhi ya wanajamii kuhusiana na madj kuwa wahuni pamoja na kukosa elimu

DJ K-Flip jina lake Halisi Calvin Michael "DJ K-Flip" likiwa linamtambulisha kazi yake anayoifanya kwa mashabiki wake wote ndani na nje ya nchi, akielezea safari yake ya kuwa DJ alisema kuwa alianza kazi hiyo mwaka 2006 kwa kuajiliwa kupiga muziki Club pamoja na Radio ijini Arusha

Club ambazo alifanya nazo kazi jijini huko ni pamoja na Triple A,Club AQ na  huku akiugawa muda wake kwa kuwahakikisha anatoa burudani kwa mashabiki wake wote kwa kutumia radio ya Triple A

Alifanya kazi jijini hapo takribani miaka minne ndipo alipoamua kujiunga na kundi la madj wa Pro 24 huku akiwa na ndoto lukuki za kufanya kazi kama team ili aweze kukabiliana na changamoto

“Kilichonisukuma kujiunga na kundi hilo ni kwa sababu nilikuwa napenda kufanya kazi kama ‘Team’ kundi kwani kwa kufanya kazi kwa kushirikiana unaongeza ujuzi na pia kunakuwa na chanagamoto ambazo ukizitumia zina kuinua kiwango “ alisema Calvin

Calvin alisema baada ya kujiunga katika kundi hilo amepata mabadiliko makubwa kwa kuongeza ujuzi siku hadi siku kwa kuwa ndani ya kundi hilo kuna mafunzo ambayo yanatolewa kwa ajili ya kuboresha ujuzi

Akizungumzia kundi hilo la Pro-24 Dj’s anasema kuwa ni kundi ambalo lina mategemeo ya kusaidia vijana hususani wenye kipaji cha kuwa Dj kwa kutoa mafunzo yatakayo msababisha Dj kuujua muziki na kujua ni aina gani ya muziki upige kulingana na mazingira yaliyopo

Anasema tangu alipojiunga na kundi hilo amekuwa akipiga muziki sehemu mbalimbali hali hiyo imemsababisha kujiongezea mashabiki wengi ambao wengi wao wameonekana kupenda kazi yake anayoifanya

Kwa hivi sasa Dj huyo anapiga sehemu tofauti tofauti zikiwemo Club Bilicans, Maisha , Masai , Savannah Lounge jijini Dar es Salaam ingawa pia anapiga katika mikoa mbalimbali pale anapohitajika kufanya hivyo hii yote ni kwa ajili ya kuwapa radha mashabiki Tanzania nzima

Anasema kuwa amekuwa na tofauti kubwa kabla ya kujiunga na kundi hilo kwani hapo mwanzo alikuwa ni Dj wa Club pamoja na Radio, wakati sasa ni tofauti amekuwa akifanya vipi tofauti tofauti kwenye televisheni

DJ K-Flip pia amekuwa akifanya shoo katika vipindi vya televisheni tofauti tofauti huku akiongezewa ujuzi na kundi hilo la Pro- 24 kwani nia yao ni kutoa burudani kwa mashabiki wao

Anafanya shoo ndani ya Clouds TV katika kipindi kinachojulikana D'Wikend Chat-Show kinachorushwa kila siku ya Ijumaa, pia anafanya shoo katika Terevisheni ya Taifa (TBC 1) kinachorushwa kila siku ya Alhamisi kikiwa kinadondoshwa na kundi zima la Pro 24

Dj K-Flip anakubali kupata usumbufu kutoka kwa mashabiki wake lakini kwa kuwa anajali kazi yake na ili asiwapoteze mashabiki wake anaamini kuheshimu kile anachokifanya kwa kumuheshimu kila shabiki na kufuata maadili ya kazi yake

Anasema kuwa msingi mkubwa wa kukwepa vishawishi ni kufuata maadili ya kazi ikiwemo kuheshimu sehemu ya kazi ili uweze kufikisha kile unachokikusudia kwa jamii nzima bila ya kupoteza maadili ya kazi pamoja na nchi

Anaongezea kuwa kazi ya DJ si ya kiuni kama watu wanavyofikilia, kwa upande wao anasema kuwa kwao ni ajila na wanaheshimu ajila hiyo kwa sababu wanapata kipato na kuendeleza maisha yao kutokana na kile wanachokifanya

Calvin anaeleza kuwa kunatofauti ya mashabiki, akizungumzia utofauti huo anasema kuwa mashabiki wa Club hawajamsababishia madhara tofauti na mashabiki wa televisheni kwani wamekuwa mtaani kwa sababu wanamuona akiwa anafanya shoo hizo

Calvin anajinadi kwa kusema kuwa kila siku anawaza kufanya bora zaidi ya mwenzake kwa kuhakikisha hilo anapokuwa anafanya shoo anahakikisha kuwa kila shabiki anafurahia kile anachokipiga

“Nikipanda kwenye shoo naingia na mzuka kwa kupiga misumari ili kusababisha mizuka kwa mashabiki wangu na wakubali kile nianchokifanya “ anasema

Mbali ya kuwa Dj,pia ni mwanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM )akiwa anasomea shahada ya Fedha na Uchumi huku akiwa na ndoto lukuki za kuwa mchumi katika nchi yetu

Calvin alisema kuwa kazi yake hiyo ya Dj haiaribu ratiba yake ya masomo na cha zaidi anahakikisha anasoma kwa bidi ili aweze kufanya vizuri pamoja na kutimiza ndoto zake

Calvin anapenda sana kuchati na marafiki wa jinsi zote , hatumii kinywaji chenye kilevi chochote kwani anaamini kwa kutumia kilevi utakuwa unajiingiza katika vishawishi vingi hivyo anapendelea zaidi kunywa juice na maji

0 Response to " DJ K-FLIP MWENYE SHAHADA YA FEDHA NA UCHUMI ALIYEBOBEA KATIKA MASWALA YA MUZIKI"

Post a Comment