Latest Updates

CHRIS BROWN 'ANAUGONJWA WA AKILI' ?

Mzizi wa tabia anazozionesha mwimbaji Chris Brown zinazotokana na hasira kali na hata kumfikisha kwenye vyombo vya sheria mara kwa mara umeelezwa kuwa ni ugonjwa wa kiakili unaojulikana kwa lugha ya kitaalamu kama ‘Bipolar Disorder na PTSD (Post traumatic Stress Disorder).
Magonjwa hayo yaliwekwa wazi mahakamani Ijumaa (February 28) wakati barua kutoka Rehab ilipokuwa ikisomwa huku Chris Brown akisikiliza kwa makini akiwa amekaa karibu na mama yake Joyce Hawkins.

“Bwana Brown pia atahitaji uangalizi wa karibu wa daktari wake ili kuhakikisha kuwa hali ya kiakili ‘bipolar Disorder’. Ilisomeka sehemu ya barua hiyo. Barua hiyo pia ilizungumzia ugonjwa huo kuwa chanzo cha Chris Brown kuwa na matatizo ya kitabia.
“Bwana Brown alikuwa mkorofi na kutenda kulingana hali ya kiafya ya kiakili ambayo haikutibiwa, kutosinzia na kupumzika kwa muda mrefu, kutopata matibabu kwa usahihi na kutotibiwa PTSD.” Yalisomeka maelezo mengine.
Bipolar disorder ni ugonjwa ambao awali ulikuwa unajulikana kama manic depression, ni ugonjwa wa kiakili ambao unamfanya awe katika ‘high mood na low mood’ na kupata mabadiliko katika kulala, nguvu, kufikiria na hata kimatendo.
Watu wenye bipolar disorder wanaweza kuwa na nyakati tofauti ambapo anaweza kujisikia furaha kupitiliza na kuwa na nguvu nyingi na kuna wakati anajisikia hana furaha, haeleweki. Huenda Chris Brown alikuwa anajisikia yuko vibaya na hana furaha akaamua kutumia marijuana kwa wingi na vilevi ili kurejesha furaha yake na ukijumlisha na hasira zinazotokana na ugonjwa huo basi kinachofuata ni kuvunja sheria kwa kuwavuruga watu.

0 Response to "CHRIS BROWN 'ANAUGONJWA WA AKILI' ? "

Post a Comment