Latest Updates

BABU NJENJE ARUDI JUKWAANI BAADA YA KUUGUA KWA MUDA


                    
Mabrouk Khamis,  Jumamosi tarehe 8 March 2014 alipanda tena jukwaani na kushirikiana na bendi yake Kilimanjaro Band aliimba nyimbo kadhaa ambazo zinapendwa na wapenzi wa bendi hiyo. Babu Njenje alipata stroke tarehe 9 December 2013 wakati akijitayarisha kwenda kwenye onyesho la bendi hiyo lililokuwa lifanyike katika ukumbi wa Escape One kusherehekea siku ya Uhuru. Katika kupata stroke hiyo aliathirika mguu na mkono wa kushoto. Taratibu katika kipindi hiki amekuwa anapewa matibabu na hatimae jana akafika jukwaani na kuimba nyimbo zake. Pamoja na kuwa bado anaendelea na matibabu kwa bado hawezi kusimama na anahitaji wheelchair kusafiri, lakini Mungu ni wa kushukuriwa hadi hapa alipofika. Kwa taarifa yake mwenyewe aliwashukuru wapenzi wa Njenje na kumtaja haswa BI Salma Mtambo kwa kumwezesha kufikia hali hiyo ya afya.

0 Response to "BABU NJENJE ARUDI JUKWAANI BAADA YA KUUGUA KWA MUDA "

Post a Comment