W
Ndugu
wawili wa kiume wa familia moja wilayani Mlele mkoa wa Katavi,
wanatuhumiwa kumuua mpenzi wa mama yao kwa kumchinja, kisha kutelekeza
mwili wake porini.
Wakazi hao ambao mmoja ni mtoto mwenye umri wa miaka 16 ni wakazi wa
Kitongoji cha Milumba Kata ya Kibaoni na aliyeuawa ni Kitungulu Luhende
(65).
Inadaiwa mama yao, Sai Mponje (65) ambaye ni mjane anayeshikiliwa
na polisi kwa sasa, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Luhende, jambo
ambalo watoto hao hawakufurahishwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alitaja
watuhumiwa hao ni Nyengu Kashele (19) na nduguye mwenye umri wa miaka
16. Mtoto huyo anashikiliwa wakati Nyengu amejificha kusikojulikana.
Mwili wa marehemu uligundulika Machi 3, mwaka huu saa 3:30 asubuhi
katika milima ya kitongoji hicho cha Milumba ukiwa umeharibika.
Mwili huo uligundulika kutokana na msako uliofanywa na askari wa jadi (sungusungu) kwa kushirikiana na polisi na wananchi.
Kidavashari alisema Februari 22, mwaka huu saa 2 asubuhi,
Luhende ambaye pia ni mkazi wa kitongoji hicho cha Milumba,
alimuaga mkewe kwamba anakwenda kijiji cha Kirida ambako ana mke
mwingine.
Hata hivyo, Kamanda alidai kuwa badala ya kwenda kijijini Kirida,
aliko mke wake mwingine, kwanza alipitia nyumbani kwa rafiki yake
katika kitongoji hicho cha Milumba, aitwae Milembe Katembeni ambako
aliacha pikipiki yake yenye nambari za usajili T449 BAF.
Inadaiwa kisha alikwenda moja kwa moja kwa Sai (mama wa watuhumiwa).
Kamanda alisema tangu hapo hakuonekana hadharani hadi mwili ulipokutwa
umetelekezwa eneo la milimani huku pembeni kukiwa na leseni yake ya
udereva.
Akielezea sababu za kuanza kumtafuta, Kamanda alisema baada ya
kutorejea kwa rafiki yake kuchukua pikipiki, Katembeni aliingiwa
wasiwasi ndipo Machi 2 , mwaka huu aliamua kutoa taarifa kwa kiongozi
wa sungusungu na kisha polisi, na msako ukaanza.
0 Response to "ATOTO WAMUUA KINYAMA MPENZI WA MAMA YAO MKOANI KATAVI"
Post a Comment