Latest Updates

TUNDAMAN 'MSAMBINUNGWA ILIMUHITAJI MASOGANGE'Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tunda Man amesema kuwa ameamua kumtumia mwanadada Agnnes  'Masongange' katika video yake mpya inayojulikana kwa jina la Msambinungwa kwa sababu anaendana na video hiyo.

Akizungumza na Pro-24 Tunda Man alisema kuwa ilikuwa ni ndoto yake kufanya kazi na mwanadada huyo, ingawa alikuwa akisubili ni nyimbo gani ambayo ingeweza kuendana na yeye alivyo.

"Masogange anavitu vyote na vionjo vinavyoendana na wimbo huo, na katika video hiyo ameweza kucheza uhusika na kunogesha nyimbo hiyo" alisema Tunda Man.

Aliweka wazi kuwa hadi sasa video hiyo imegharimu zaidi ya milioni 6, ambapo gharama sahihi atazijua baada ya kukamilika kwa video hiyo ambayo inatarajia kumalizika hivi karibuni.

0 Response to "TUNDAMAN 'MSAMBINUNGWA ILIMUHITAJI MASOGANGE'"

Post a Comment