Latest Updates

KINGWENDU NAE ATUMBUKIA KWENYE SIASA ATAKA UBUNG


     

Wasanii wa fani mbalimbali kukimbilia katika siasa limezidi kushika kasi, baada ya msanii wa maigizo na vichekesho, Rashid Mwinshehe maarufu kama Kingwendu, kufunguka na kusema kuwa yupo katika mipango ya kuwania nafasi ya ubunge wakati wa Uchaguzi Mkuu wa nchi utakaofanyika 2015.


Msanii huyo mahiri ambaye licha ya vichekesho pia ni mwanamuziki, alisema hata hivyo, muda wa kusema jimbo na chama atakachokitumia kutafuta ridhaa ya wananchi hatakitaja kwa sasa, kwa kile alichodai bado anashauriana na washauri wake.

      

“Nimejipanga vya kutosha kuingia bungeni na niko kwenye mikakati mikubwa na washauri wangu wa mambo ya siasa wanaendelea kunipika, ili niive lakini habari ndiyo hiyo naomba watanzania waniombee tu ili nikawawakilishe,” alisema.
Licha ya kusema kuwa siasa ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu, alisema kwa sasa pia yupo shule, akijifunza uelewa wa mambo ya kisiasa sambamba na lugha ya kigeni, alizodai zitasaidia kumjenga.

“Ndugu mwandishi, kwa sasa sitaki kuweka wazi kuhusu chama nitakachoingia nacho bungeni na jimbo lake, lakini vuguvugu za uchaguzi zikianza tu, nitaweka wazi lakini nitaingia kwa chama kinachopendwa sana na wananchi na jimbo nitakalogombae ni hapa hapa mjini Dar,” alisema.

0 Response to "KINGWENDU NAE ATUMBUKIA KWENYE SIASA ATAKA UBUNG"

Post a Comment