Latest Updates

WATOTO 124 WAZALIWA MKESHA WA SIKUKUU YA KRISMASI DAR

Baadhi wa wazazi katika Hospitali ya Mwananyamala.
Watoto 124 wakiwemo wa kiume 80 wamezaliwa katika mkesha wa Sikukuu ya Krismasi katika hospitali za Dar es Salaam  huku wengi wakiwa wa kiume.
Watoto hao wamezaliwa katika hospitali za Muhimbili, Temeke, Mwananyamala na Amana, ambapo watoto wanne katika hospitali ya Mwananyamala walizaliwa kwa njia ya operesheni.
Mganga wa Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala,  Dk Sophinias Ngonyani alisema watoto waliozaliwa katika hospitali hiyo jumla walikuwa watoto 42,  ambapo 18 wakike na 24 wakiume .
Ngonyani alisema kuwa hakuna mtoto au mama aliyepoteza maisha katika mkesha wa Krismasi.
Katika hospitali ya Amana, walizaliwa watoto 38, ambao wakike 12 na wakiume 26.
Kwa upande wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, watoto waliozaliwa ni sita, huku kukiwa hamna aliyezaliwa kwa njia ya upasuaji.  Hospitali ya Temeke jumla ya watoto waliozaliwa ni 38, ambapo wakiume ni 24 na wa kike ni 12.
Muuguzi wa zamu wa hospitali ya Temeke, Happiness Mbalawa alisema watoto waliozaliwa kwa njia ya upasuaji hospitalini hapo ni wawili, wakiume mmoja na wakike mmoja. 
Katika hospitali zote hakuna mtoto aliyepoteza maisha au kuzaliwa na ulemavu.
 
BY DJ SEK

0 Response to "WATOTO 124 WAZALIWA MKESHA WA SIKUKUU YA KRISMASI DAR "

Post a Comment