Latest Updates

Watahiniwa 411,127 wafaulu kujiunga sekondari

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu –TAMISEMI, Jumanne Sagini (picahni) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya wanafunzi 411,127 kati ya 427,609 sawa na asilimia 96.15 waliofaulu mtihani wa darasa la saba 2013  wataanza kidato cha kwanza mwaka ujao.
Kati  yao  wasichana ni 201,021 na wavulana 210,106 na huku kiwango cha wanafunzi waliochaguliwa mwaka huu wakiwa wameongezeka kwa asilimia 31.37 ikilinganishwa na asilimia 64.78 waliochaguliwa awamu ya kwanza mwaka huu.
Matokeo yanaonesha kuwa jumla ya wanafunzi 427,609 (wavulana 218,093 na wasichana 209.516) walifaulu kwa kupata alama A-C kati ya 844,938 waliofanya mtihani ikiwa ni sawa na asilimia 50.61 … takwimu zinaonesha ongezeko la asilimia 19 la ufaulu ikilinganishwa na asilimia 30.6 mwaka jana.
 
 
BY DJ SEK

0 Response to "Watahiniwa 411,127 wafaulu kujiunga sekondari"

Post a Comment