Latest Updates

DARASA ATOKA NA MIXTAPE VOL 1.MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Darasa amefanikiwa kuachia kanda mseto 'Mixtape' yenye nyimbo 19 aliyoipa jina la 'Dream Big-Chapakazi' ikiwa inasauti za wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya akiwemo Shilole, Ngwear, Mchizi Moxie.
Akielezea dhumuni la kuachia kanda mseto hiyo alidai kuwa ni moja ya kuupeleka muziki mtaani huku akiwahimiza vijana kuutumia muziki huo kwa nia ya kujikomboa.
Alidai kuwa kanda hiyo itasambazwa nchi nzima ili ujumbe ufike kwa jamii nzima hususani vijana ili waweze kuutumia muziki huo kwa lengo la kujikomboa na kuutendea kazi muziki huo.
Mbali na hilo alidai kuwa bado anaendelea kutoa fulsa kwa vijana katika kuukuza muziki huo kwa kutoa nafasi kwa baadhi ya vijana ambao wapo mitaani kwa  kushirikiana kufanya nao kazi ambazo zitaingia katika kanda hiyo.
Alidai kuwa ameamua kuanzisha utaratibu huo wa kuwashirikisha vijana katika kazi hiyo ili kutoa nafasi kwa vijana hao ambao wanavipaji ila bado hawajapata fursa ya kukuza vipaji vyao.

0 Response to "DARASA ATOKA NA MIXTAPE VOL 1. "

Post a Comment